Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Oktoba 09 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Oct 2024
Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Oktoba 09 2024

Kevin de Bruyne huenda akahamia Al-Nassr ya Saudi Arabia, Liverpool wana matumaini ya kusalia na Trent Alexander-Arnold huku klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England zikivutiwa na mchezaji wa Bournemouth Antoine Semenyo

Klabu ya Saudia Al-Nassr ina matumaini ya kumsajili kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Team Talk)

Beki wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, 26, anaweza kushawishika kumaliza kandarasi yake Anfield ili kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure na kuungana na mchezaji mwenzake wa Uingereza Jude Bellingham. (Sun)

Mshambulizi wa Bournemouth Antoine Semenyo, 24, anawaniwa na klabu za Liverpool, Newcastle United na Tottenham baada ya mchezaji huyo raia wa Ghana kuanza vyema msimu huu. (Give Me Sport)

Real Madrid wameimarisha mpango wa kumnunua Alexander-Arnold lakini Liverpool wanatumai wanaweza kumshawishi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kusalia katika klabu hiyo. (Football Insider)

Liverpool wamemtambua mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt wa Misri Omar Marmoush, 25, na mshambuliaji wa Borussia Dortmund wa Ujerumani Karim Adeyemi, 22, kama mbadala wa winga wa Misri Mohamed Salah, 32. (Sky Germany - kwa Kijerumani)

Matumaini ya Manchester United ya kumsajili kiungo wa Colombia Richard Rios yameimarika, huku Palmeiras ikiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa euro milioni 20 mwezi Januari. (Caught Offside)

Arsenal na Manchester United wanamfuatilia mlinda lango wa Wigan Athletic Muingereza Sam Tickle mwenye umri wa miaka 22. (Team Talk)

Uongozi wa Southampton unatazamiwa kukutana ili kujadili mustakabali wa kocha Russell Martin katika klabu hiyo. (Football Insider)

Mshambulizi wa Paris St-Germain na Ufaransa Randal Kolo Muani, 25, anaweza kuhama klabu hiyo mwezi Januari lakini mabingwa hao wa Ligue 1 wanataka kumuuza kwa angalau euro milioni 70. (AS - kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 21, ana nia ya kujiunga na Bayern Munich msimu ujao. (Sky Germany - kwa Kijerumani)

Newcastle United wanaendelea kumfuatilia mshambuliaji wa Lille na Canada Jonathan David, 24, kwa lengo la uhamisho wa Januari. (Football Insider)

Hugo Viana, mkurugenzi wa soka katika klabu ya Sporting ya Ureno, ndiye mgombea anayependekezwa na Manchester City kuchukua nafasi ya Txiki Begiristain anatarajiwa kujiunga mabingwa wa Ligi Kuu ya England. (Fabrizio Romano)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’