Yanga - Simba - Azam - Singida - Local

Magoli 91 yafungwa NBC PL

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Oct 2024
Magoli 91 yafungwa NBC PL

Jumla ya mabao 91 yamefungwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Mabao hayo yamefungwa katika michezo 50 ambayo imechezwa mpaka sasa wakati ligi hiyo imesimama kupisha michezo ya kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025)

Mabao hayo yamefungwa na idadi ya wachezaji 65, huku, straika wa Fountain Gate, Selemani Mwalimu akiwa kinara, akipachika magoli matano mpaka sasa

Takwimu zinaonyesha kati ya mabao hayo, 10 yamefungwa kwa penalti na moja la kujifunga. Waliofunga mabao kwa penalti ni Djuma Shaaban wa Namungo, Heritier Makambo na Shedrack Asiegbu (Tabora United), Jean Ahoua na Leonel Ateba (Simba), Ibrahim Elias (KMC), Salum Kihimbwa (Fountaina Gate), Hassan Dilunga (JKT Tanzania), Nurdin Chona (Prisons) na Stephane Aziz Ki wa Yanga

Fred Tangalo wa KMC, alijifunga katika harakati za kuokoa katika mchezo ulichezwa Septemba 19, mwaka huu wakati timu yake ikipata kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Azam FC, likiwa ni bao pekee la kujifunga tangu kuanza kwa msimu huu

Katika mabao hayo 91, Fountain Gate ndiyo iliyofunga mengi zaidi mpaka sasa, ikipachika mabao 14, ikifuatiwa na Simba yenye mabao 12, huku Pamba Jiji ikifunga mabao mawili tu ambayo ni machache zaidi kufungwa na timu kwenye ligi mpaka sasa

Takwimu zinaonyesha katika michezo 50 ya Ligi Kuu iliyochezwa mpaka sasa, 33 imetoa washindi na 17 imemalizika kwa sare. Pia katika michezo 33 ya ushindi, mechi 19 timu zimeshinda zikicheza viwanja vya nyumbani, na michezo 14 imetoa washindi timu zikicheza ugenini

Ratiba inaonyesha Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea tena Oktoba 18, mwaka huu ambapo michezo ya raundi ya nane itaanza, Coastal Union itaikaribisha Dodoma Jiji, JKT Tanzania itakuwa mwenyeji wa Tabora United na Prisons itakuwa nyumbani dhidi ya Azam FC

Oktoba 19, kutakuwa na patashika nguo kuchanika miamba miwili ya soka nchini, Simba ya Yanga zitavaana, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, huku Oktoba 20, Singida Black Stars itacheza dhidi ya Namungo na Fountain Gate itawaalika KMC

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’