Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo inashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kumenyana na DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2025
Katika kuhakikisha timu inapata sapoti kubwa ya mashabiki, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk Samia Suluhu Hassan amenunua tiketi 20,000 za Mzunguuko kwa ajili ya mashabiki kuingia bure. Mapema Azam TV na Wadhamini wengine walilipia tiketi 10,000
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Gerson Msigwa amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa leo kuipa hamasa timu yao ya Taifa katika mchezo ambao Tanzania inahitaji ushindi
Ili kuweka hai matumaini ya kufuzu Afcon 2025, Stars inahitaji kushinda mchezo dhidi ya DR Congo leo
Itakuwa mechi ngumu kwa sababu DR Congo nao wanahitaji ushindi ili kujihakikishia tiketi ya kufuzu mapema
Kaimu Kocha Mkuu wa Tanzania Hamed Morocco amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo na watapambana kuhakikisha wanaibuka na ushindi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi wa mchezo huo ambao pia Rais Mstaafu Awamu ya nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete ataushuhudia katika dimba la Mkapa



