Kaze aungana na Nabi Kaizer Chiefs

Joel JJ By Joel JJ β€’ 17th October 2024


Kaze aungana na Nabi Kaizer Chiefs

Klabu ya Kaizer Chiefs imemteua Cedric Kaze kuwa kocha msaidizi akiungana na kocha Nasreddine Nabi waliofanya kazi pamoja Yanga kwa misimu miwili

Inaelezwa Nabi aliwataka mabosi wake wamuajiri Kaze ili kuongeza nguvu katika benchi lake la ufundi

Akiwa na Nabi katika kikosi cha Yanga, walishinda mataji sita katika misimu miwili pamoja na kucheza fainali ya kombe la Shirikisho la CAF

Tangu atue Kaizer Chiefs, Nabi amefanikiwa kuwaongeza katika benchi lake la ufundi Kaze na Khalil Ben Youssef ambao alifanya nao kazi Yanga


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.