Yanga - Local

Tutawaheshimu Simba - Gamondi

Joel JJ By Joel JJ
18 Oct 2024
Tutawaheshimu Simba - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba yamekamilika na wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na furaha

Gamondi amesema kikosi chake hakikuwa na jambo jipya katika maandalizi kwani mechi dhidi ya Simba haina tofauti na mechi nyingine walizocheza kwenye ligi

"Tuna furaha kubwa kuelekea kwenye ligi huku tukiwa na mchezo muhimu wa Derby. Tupo vizuri, tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri hapo kesho. Hatujabadilika sana kwenye maandalizi tumejiandaa kama ambavyo tumekuwa tukifanya hapo awali:

"Tumetokea kwenye wiki ya FIFA na mara nyingi tunapata changamoto kidogo ya maandalizi kwani wachezaji wetu wengi wanakuwa kwenye majukumu ya timu za TAIFA"

"Kwa mfano kuna wachezaji wamefika jana na wengine wanaingia leo kwa mantiki hiyo lazima upate ugumu kwenye maandalizi lakini tutafanya kila liwezekanalo," alisema Gamondi

Gamondi amesema anatarajia mchezo huo utakuwa mzuri na kuwapa burudani mashabiki watakaojitokeza kushuhudia

"Tunawaheshimu Simba, ni timu nzuri yenye wachezaji na kocha mzuri. Naamini itakuwa mechi nzuri yenye ushindani na kuwapa burudani mashabiki"

"Nafikiri ni jambo zuri kwa soka la Tanzania kuwa na aina ya mechi hii yenye ushindani ambayo naamini itazidi kulitangaza soka la Tanzania," aliongeza Gamondi

Aidha Gamondi amethibitisha kikosi chake kiko kamili na hakuna mchezaji wake muhimu ambaye atakosekana

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
5h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
6h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
8h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
8h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
9h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
9h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
9h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
9h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
10h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
12h ago
READ MORE →