Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Crescentius Magori amemshushia lawama mwamuzi Ramadhan Kayoko kwa kuinyima Simba penati mbili halali katika mchezo dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Magori pia alieleza kutofurahishwa na aina ya faulo waliyopewa Yanga ambayo ilipelekea kufungwa kwa bao hilo alilojifunga beki Kelvin Kijili katika jitihada za kuokoa shuti la Maxi Nzengeli
Hakuishia hapo, Mtendaji Mkuu huyo wa zamani wa Simba, alimshushia tuhuma mlinda lango Mussa Camara
"Musa Camara, Musa Camara nakuita mara 3!! Tutajua very soon! Hata huko Conakry tutafika! Kayoko Kibu kaangushwa mara 2 ndani ya 18 hukutoa penati unaenda kutoa faulo haina kichwa wala miguu," aliandika Magori katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Nae Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu amesema waamuzi waliharibu mechi hiyo kwa kuinyima Simba faida katika matukio muhimu