Yanga - Simba - Local

Gamondi ameweka rekodi dhidi ya Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Oct 2024
Gamondi ameweka rekodi dhidi ya Simba

Jana Yanga ilijihakikishia ushindi wa nne mfululizo dhidi ya watani zao Simba katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Bao la kujifunga Simba dakika ya 86 baada ya shuti la Maxi Nzengeli kumgonga Kelvin Kijili, lilitosha kuihakikishia Yanga ushindi wa tano mfululizo katika ligi msimu huu na kupanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amedhihirisha ubora wake mbele ya Simba kikosi chake kikiweka rekodi ya kugawa vipigo vinne mfululizo kwa watani

Yanga ilianza mchezo huo taratibu na kuwapa Simba nafasi ya kumiliki mchezo katika dakika 25-30 za kipindi cha kwanza

Gamondi alisema ulikuwa mkakati wao wa kimbinu kuanza hivyo kwa sababu alifahamu Simba wangeanza mchezo huo kwa kasi huku pia kikosi chake kilikabiliwa na changamoto ya uchovu kwa baadhi ya wachezaji waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa

"Baadhi ya wachezaji walifika siku moja kabla ya mchezo na wengine walirudi Alfajiri ya siku ya mchezo, utaona ni kwa kiasi gani tulikuwa na changamoto kubwa katika maandalizi yetu"

"Tulicheza kwa tahadhari kubwa katika kipindi cha kwanza tukifahamu wapinzani wetu wataanza na kasi kubwa lakini kipindi cha pili tulifanya mabadiliko ya kimbinu, tukamiliki mchezo nadhani tulistahili kushinda"

"Nawapongeza wachezaji wangu haikuwa mechi nyepesi, ushindi huu ni matokeo ya ari ya kujituma kwao kwa dakika zote 90 za mchezo," alisema Gamondi

Kuingia kwa Kennedy Musonda, Clement Mzize na Clatous Chama kulibadili taswira ya mchezo ambapo Yanga iliongeza kasi ya mashambulizi kupelekea kupata bao hilo dakika za jiooooooooni

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’