Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu, Oktoba 21 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Oct 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu, Oktoba 21 2024

Everton wako tayari kumnunua winga wa AC Milan, Samuel Chukwueze, Manchester United wana matumaini ya kumsajili Alphonso Davies, Dusan Vlahovic bado anaweza kuhamia Arsenal. Everton wanapanga kumsajili winga wa AC Milan kutoka Nigeria Samuel Chukwueze, 25, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Football Insider)

Manchester United wanalenga kumshawishi beki wa pembeni wa Bayern Munich Alphonso Davies, 23, kuwachagua badala ya Real Madrid mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Kanada utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. (Fichajes - kwa Kihispania)

Arsenal wanaweza kumpata Mserbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 24, baada ya kumsaka kwa muda mrefu kwa bei nafuu kwa sababu mazungumzo ya mshambuliaji huyo wa Juventus na klabu yake kuhusu kandarasi mpya hayaendelei vizuri.(Caught Offside)

Meneja ajaye wa England Thomas Tuchel ametengana na mshirika wake wa muda mrefu wa ukufunzi Zsolt Low kabla ya kuchukua nafasi yake huko Three Lions. (Sun)

Aston Villa wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25, kutoka Brentford . (TBR Football)

Manchester United huenda huenda wakamuachilia kwa mkopo mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 23, kwa Juventus ikiwa watamsajili mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 21, msimu ujao. (Tuttomercato - kwa Kiitaliano)

Manchester City, Liverpool , na Tottenham wameelekeza macho yao kwa winga wa Real Valladolid Mhispania Raul Moro, 21. (Fichajes – kwa Kihispania)

Winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jamie Bynoe-Gittens, 20, amezivutia Arsenal, Tottenham, Crystal Palace na Nottingham Forest - ingawa klabu hiyo ya Ujerumani inataka zaidi ya £50m kwa mchezaji huyo kabla ya kufikiria kumuuza. (Caught Offside)

Arsenal, Juventus, AC Milan na Napoli ni miongoni mwa vilabu vinavyomtazama kiungo wa kati wa Como na Argentina Nico Paz, 20. (Nicolo Schira on X)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’