Klabu ya Soka ya Tabora United, imetangaza kuachana na aliyekuwa Kocha wao mkuu, Francis Kimanzi pamoja na aliyekuwa msaidizi wake Yusuph Chipo
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, uamuzi huo umechukuliwa kutokana na mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu wa 2024/24
Tabora United inashika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi ikikusanya alama 8 baada ya kushinda mechi mbili na kutoka sare mechi mbili
Wafuga nyuki hao wamepoteza mechi nne katika ya nane walizocheza mpaka sasa



