Bayern Munich na Marseille wameungana na Paris St-Germain katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 26, kutoka Manchester United. (Tea Talk) Manchester United wako tayari kupokea ofa za mkopo kwa ajili ya winga wa Brazil Antony, 24 wakati wa usajili wa Januari. (Football Insider)
Gwiji mstaafu wa Italia na Roma Francesco Totti, 48, anasema huenda akarejea uwanjani baada ya kuwasiliana na klabu kadhaa za Serie A. (Gazzetta Dello Sport - kwa Kiitaliano)
Arsenal, Aston Villa na Newcastle wanavutiwa na kiungo mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Oscar Gloukh, 20. (Caught Offside)
Bayer Leverkusen wanajiandaa kwa ajili ya kuondoka kwa kocha Xabi Alonso msimu ujao, huku Mhispania huyo akinyatiwa na Real Madrid na Manchester City, iwapo Pep Guardiola ataamua ataondoka. (Sky Germany)
Everton wanaandaa dau la pauni milioni 17 kumnunua mshambuliaji wa Besiktas wa miaka 19 wa Uturuki Semih Kilicsoy. (Kontraspor - kwa Kituruki)
La Liga inaomba Shirikisho la Soka la Uhispania, Uefa na Fifa kuruhusu mchezo wa Barcelona dhidi ya Atletico Madrid wa mwezi Desemba kufanyika Miami. (Mail)
Arsenal wanatafuta mbinu za kupanua Uwanja wa Emirates. (Times - usajili unahitajika)
BBC



