Local,Normal News,Simba

Tumepoteza derby sio ubingwa - Ahmed

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Oct 2024
Tumepoteza derby sio ubingwa - Ahmed

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema kupoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya watani zao Yanga hakuwezi kuwatoa katika mipango yao ya kuwania ubingwa msimu huu

Oktoba 19 Simba ilichapwa bao 1-0 na Yanga katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, matokeo ambayo ni kama yamewakatisha tamaa mashabiki wa timu hiyo

Ahmed amesema kila Mwanasimba ameumizwa na matokeo hayo lakini wana matumaini katika malengo yao kwa sababu bado safari ni ndefu kukamilisha msimu huu

Msemaji huyo wa Simba amesema licha ya kupoteza mchezo huo, project yao ya kujenga Simba imara imeanza kuonyesha matunda

"Tunaumia kwa kupoteza mchezo wa derby lakini tunajipongeza kwa kuwa mradi wetu wa kutengeneza timu umeanza kutoa matunda tena kwa haraka sana"

"Wote ni mashahidi misimu kadhaa nyuma tulifungwa derby na kuzidiwa kwa dakika zote 90. Tumeona tofauti kubwa, tumefungwa lakini tumeutawala mchezo kwa asilimia kubwa na kama kila kitu kingekua sawa basi tungeshinda mchezo ule"

"Muhimu kwetu wana Simba kwanza tukubali tumepoteza na wala hakuna haja ya kuanza kuhesabu tumepoteza mara ngapi, mpira ni maisha ya duara muda wetu utafika na sisi tutatawala derby kwani tumewahi kufanya hivyo"

"Muhimu kwa sasa ni kusahau yaliyotokea na kujipanga upya kwa vita iliyo mbele yetu. Tumebakiwa na michezo 24 nguvu kubwa iwe kushinda michezo hiyo, tumepoteza derby sio ubingwa," alisema Ahmed

Leo Simba iko mkoani Mbeya kumenyana na Tanzania Prisons katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya NBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
45m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’