Yanga - Local

Diarra afichua alivyoiwahi Kariakoo Derby

Joel JJ By Joel JJ
22 Oct 2024
Diarra afichua alivyoiwahi Kariakoo Derby

Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra amesema mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Benjamin Mkapa, ni moja ya mechi zilizoingia katika kumbukumbu ya maisha yake ya soka katika ardhi ya Tanzania

Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo ambao Diarra amefichua kuwa alishuka uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius Nyerere na moja kwa moja kuelekea uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza mchezo huo

"Mechi yangu bora ya Simba na Yanga tangu nifike hapa ni hii ya juzi ya ushindi wa bao 1-0 kwa sababu nilifika Tanzania siku ya mechi"

"Nashukuru sana tuliweza kushinda, kwa kweli hii inabaki kuwa mechi yangu bora sana," alisema Diarra

Diarra amemshukuru Rais wa Yanga kwa kuhakikisha anafanya kila linalowezekana ili awahi mchezo huo akiwa ametoka katika majukumu ya timu ya Taifa ya Mali

"Rais alinitengenezea mazingira mazuri ya usafiri, sikuchoka kwani nilipata tiketi ya Business Class"

"Nilivyotua uwanja wa ndege alituma mtu anifuate ili niwahi moja kwa moja uwanjani. Kama kuna siku niliuwazia ushindi basi ni siku ile," aliongeza Diarra

Akizungumzia tukio la kuinusuru Yanga kufungwa bao la mapema katika mchezo dhidi ya Simba, Diarra alisema amekuwa akiifuatilia Simba katika mechi zao hivyo alikuwa na ufahamu juu ya maamuzi ya mshambuliaji Lionel Ateba

"Huwa naangalia mechi za Simba kwa hiyo nawajua. Nilimuona (Ateba) anavyocheza, nilifahamu akipata mpira eneo lile atafanya nini, nilijua ataenda kushoto na sikuwa na presha"

"Nilivyookoa sikuhama eneo nikasimama vilevile kwani nilijua mpinzani atapiga nikaokoa tena," alisema Diarra

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
1h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
3h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
3h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
3h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
3h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
5h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →