Klabu ya Coastal Union imemtangaza Juma Mwambusi kocha wake mkuu akisaini mkataba wa mwaka mmoja
Taarifa iliyotolewa na Coastal Union katika ukurasa wa mtandao wa kijamii imethibitisha kutua kwa kocha huyo aliyewahi kuzinoa klabu za Mbeya City, Yanga na Ihefu kama kocha mkuu na Azam Fc kama kocha msaidizi
"Ubora,weledi,mipango,mikakati na uwezo wako kila Mtanzania anaujua. Sasa malengo yetu ya kumaliza moja kati ya nafasi nne za juu yanakwenda kutimia 100%"
"Karibu sana mwalimu Juma Mwambusi, standard yako ni kufundisha klabu kubwa na kongwe hapa nchini"
"Wanamangushi Wanajua uwezo wako na spirit yako ya kupambania alama 3 kwa kila mchezo. Karibu mkuu wa benchi la ufundi na kocha mkuu Juma Mwambusi," ilibainisha taarifa ya Coastal Union

