Kocha Mkuu Yanga Miguel Gamondi amewapongeza wachezaji wake baada ya kucheza mechi 16 mfululizo za ligi bila ya kupoteza
Jana Yanga iliichapa JKT Tanzania mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Akizungumza baada ya mchezo huo Gamondi alisema sio kazi rahisi kucheza mechi 16 za ligi bila kupoteza lakini imewezekana kutokana na ubora wa wachezaji alionao
"Nawapongeza wachezaji wangu kwa ushindi wa leo (jana), tumecheza mechi 16 za ligi (tangu msimu uliopita) tumeshinda 15, sare 1 tukipata cleensheet 12 katika mechi hizo"
"Tumefanya mabadiliko ya kikosi katika baadhi ya maeneo tukiwapumzisha wachezaji waliotumika mchezo uliopita na kuwapa nafasi ambao hawakucheza dhidi ya Simba"
"Tunakabiliwa na ratiba ya mechi mfululizo ambayo inatulazimu kufanya hivyo, tutacheza Jumamosi dhidi ya Coastal Union na pia tutacheza Jumatano (ijayo) dhidi ya Singida BS"
"Tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha tunazidi kufanya vizuri katika mechi zinazofuata," alisema Gamondi
Ni mwendo wa rekodi kwa Yanga kwani sasa Wananchi wamecheza jumla ya mechi 26 katika mashindano yote (ukiacha mechi za kirafiki) mechi 16 zikiwa za ligi kuu
Mara ya mwisho Yanga kupoteza ni mechi ya mashindano ni 05/04/2024 dhidi ya Mamelod Sundowns mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya ligi ya mabingwa
Yanga walipoteza mchezo kwa mikwaju ya penati 3-2 baada ya suluhu ya bila kufungana kwa dakika 180. Hata hivyo ni mchezo ambao Mamelodi walinufaika na makosa ya kibinadanu ya Mwamuzi