Kiungo wa zamani wa Arsenal na timu ya Taifa ya Uingereza, Jack Wilshere ameacha nafasi yake kama kocha mkuu wa kikosi cha U18 cha Arsenal na kujiunga na Norwich City katika nafasi ya ukocha wa kikosi cha kwanza
Wilshere, 32, alirejea katika klabu yake ya zamani mnamo Julai 2022 kama kocha mkuu wa Vijana wa U18 wa Arsenal na kuwaongoza hadi fainali ya Kombe la FA kwa Vijana, ambapo walishindwa na West Ham
Mkurugenzi wa michezo wa Norwich Ben Knapper anamfahamu Wilshere tangu alipokuwa meneja wa masuala ya mikopo Arsenal
Wilshere alikaa Arsenal kwa miaka miwili lakini sasa anaona kuhamia Norwich kama hatua nzuri zaidi katika maisha yake ya ukocha.