Barcelona yaifumua Bayern 4-1

ProSports Media By ProSports Media β€’ 24th October 2024


Barcelona yaifumua Bayern 4-1

Kiungo mshambuliaji Raphinha aliibuka nyota wa mchezo ligi ya mabingwa akifunga hat-trick katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Bayern Munich kwenye Mechi 3

Fowadi huyo wa Brazil alifunga hat-trick, likiwemo bao baada ya sekunde 56 pekee; goli la haraka zaidi kuwahi kufungwa na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa

Huku kukiwa na mabao mengine dakika ya 45 na 56, Raphinha amekuwa mchezaji wa nne kufunga hat-trick kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich baada ya Roy Makaay, Sergio Agüero na Cristiano Ronaldo

Harry Kane aliifungia Bayern bao lakufutia machozi likiwa ni ao lake la 34 la UEFA Champions League, na hivyo kuongeza rekodi yake ya kuwa mfungaji bora wa mabao wa Uingereza kwenye mashindano hayo

Mshambulizi wa zamani wa Bayern Robert Lewandowski aliiweka Barcelona mbele dakika 16 tu baadaye. Fowadi huyo wa Poland alifunga bao lake la 97 katika mashindano hayo, na hivyo kumfanya asalie mabao matatu pekee kutoka kuwa mchezaji wa tatu kufikisha magoli ya UCL kwa karne baada ya Ronaldo na Lionel Messi

Kwa Bayern, hii iliwapa ladha ya dawa yao baada ya kuwacharaza Dinamo Zagreb kwenye MD 1 (9-2), lakini Barcelona walikuwa katika kiwango bora usiku wa kuamkia leo

Mechi yao inayofuata ni El Clasico Jumamosi dhidi ya Real Madrid katika uwanja wa Bernabeu


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.