Kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market, mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland na kiungo mshambuliaji wa Real Madrid Vinicious Junior ndio wachezaji ghali zaidi duniani kwa sasa
Wachezaji hao kila mmoja ana thamani ya Pauni Mil 200 wakifuatiwa na Jude Bellingham wa Real Madrid mwenye thamani ya Pauni Mil 180 kama ilivyo kwa Kylian Mbappe wa Real Madrid pia
Winga kinda wa Barcelona Lamine Yamal anashika nafasi ya tano akiwa na thamani ya Pauni Mil 150
Katika orodha hiyo, wachezaji watatu ghali zaidi duniani wanatoka klabu ya Real Madrid




