Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika (ACA) Injinia Hersi Ally Said ameshinda Tuzo ya Mwanamichezo mwenye mchango kwenye maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika
Sherehe za utolewaji tuzo hizo za Nigeria-France Sports Awards, zilifanyika jijini Paris, Ufaransa, juzi
Tuzo ya Injinia Hersi ilipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Mhe.Ali Jabir Mwadini



