Singida BS, Simba, Azam vitani NBC PL

Joel JJ By Joel JJ β€’ 25th October 2024


Singida BS, Simba, Azam vitani NBC PL

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi tatu zinatarajiwa kupigwa katika viwanja mbalimbali

Vinara wa ligi hiyo Singida BS, saa 8 mchana watakuwa uwanja wa nyumbani CCM Liti kuwakaribisha wapinzani wao wakuu Fountain Gate. Hii ni Derby ya mapacha ambayo inapigwa mapema

Hata hivyo Fountain Gate wanakwenda kwenye mchezo huo bila ya huduma ya wachezaji wao mauhimu, Selemani Mwalimu ambaye ni kinara wa ufungaji msimu huu akiwa na mabao 6 na Edgar William ambaye anashika nafasi ya pili akiwa na mabao manne

Wachezaji hao wamejumuishwa kikosi cha timu ya Taifa wachezaji wa ndani kinachotarajiwa kucheza dhidi ya Sudan Oktoba 27

Saa 10:15 jioni mchezo mwingine mkali kati ya Simba dhidi ya Namungo Fc utapigwa katika uwanja wa KMC Complex jijini Dar es salaam

Simba inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi itakuwa ikisaka alama tatu ambazo zinaweza kuwasogeza juu ya watani zao Yanga katika msimamo wa ligi

Hata hivyo wanakwenda kukutana na Namungo Fc ambayo juzi ilimtangaza Juma Mgunda kuwa kocha wake mkuu

Mgunda amefanya kazi Simba kwa takribani misimu mitatu hivyo unaweza kusema anawajua vyema waajiri wake hao wa zamani

Saa 1 usiku Azam Fc itakuwa uwanja wa nyumbani, Azam Complex kuumana na KenGold inayoburuza mkia katika msimamo wa ligi


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.