Mkufunzi wa Fenerbahce Jose Mourinho alitolewa kwa kadi nyekundu wakati timu nyake ikitoka nyuma na kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya klabu yake ya zamani Manchester United katika mchezo wa ligi ya Europa
Kwa Manchester United, hiyo ilikuwa ni sare ya tatu mfululizo katika michuano hiyo
United walikuwa wameongoza kipindi cha mapumziko kupitia bao la nne la Christian Eriksen msimu huu
Lakini wenyeji walisawazisha dakika nne baada ya mchezo kuanza kipindi cha pili wakati Youssef En-Nesyri alipowahadaa walinzi wa United na kufunga kwa kichwa krosi ya Allan Saint-Maximin
Mourinho alikumbwa na mkasa wa 'kula umeme' mbele ya mwamuzi Mfaransa Clement Turpin wakati akilalamikia mkwaju wa penati baada ya Bright Osayi-Samuel kuangushwa katika eneo la hatari

Licha ya maandamano ya hasira kutoka kwa benchi ya Fenerbahce, VAR iliunga mkono maoni ya Turpin hakuna chochote kinyume cha sheria kuhusu tukio hilo na Turpin alikuja eneo la kiufundi kumuamuru Mourinho aondoke
United walipata nafasi za kushinda mchezo huo lakini Rasmus Hojlund aliamua kwenda peke yake badala ya kumpasia Alejandro Garnacho na mkwaju wake ukampita kipa wa Fenerbahce Dominik Livakovic bila madhara