Local,Normal News,Yanga, Coastal

Ratiba yamvuruga Gamondi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Oct 2024
Ratiba yamvuruga Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameitaka Bodi ya Ligi kuzingatia afya za wachezaji inapoandaa ratiba ya mechi za ligi kuu ya NBC

Gamondi ametoa malalamiko hayo wakati akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo wa ligi kuu kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga utakaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jumamosi Oktoba 26

Gamondi amesema hawana muda wa kufanya maandalizi ya mechi na wachezaji kupumzika kwa sababu ratiba inawalazimu kucheza kila baada ya siku tatu

"Wanaoandaa kalenda wanatakiwa wafahamu wachezaji sio maroboti ni binadamu na hata Ulaya tayari wameanza kuilalamika FIFA kuwa na ratiba inayobana mechi nyingi za ligi ya mabingwa na hiyo imeanza na hapa"

"Madhara ya hayo yote ni majeraha kwa wachezaji na italeta athari kwa wachezaji na ubora wa mechi kupungua"

"Tunacheza mechi ambayo wapinzani wetu wanajiaandaa kwa siku 7 mpaka 8 lakini sisi tunafanya mambo ndani ya muda mchache"

"Yasichukuliwe kama malalamiko lakini yawe ni kama maboresho kwa watu wanaoandaa kalenda kwa manufaa ya ligi,"alisema Gamondi

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo huo, Gamondi alisema anatarajia mchezo hautakuwa mwepesi, akihofia uwanja hautawaruhusu kucheza aina yao ya soka

"Tunategemea itakuwa mechi ngumu kwa kuzingatia uwanja pia hauruhusu kucheza aina yetu ya mpira lakini tutajitahidi kufanya kile kinachowezekana na tumekuja hapa tukiwa na malengo ya kushinda mechi," aliongeza Gamondi

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’