Local,Normal News,Simba, Namungo

Simba yaifunza soka Namungo Fc, yaichapa 3-0

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Oct 2024
Simba yaifunza soka Namungo Fc, yaichapa 3-0

Wekundu wa Msimbazi Simba Sc wameendeleza ubabe wao katika uwanja wa KMC Complex wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Ulikuwa mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi, pengine mambo yangekuwa mabaya zaidi kwa Namungo Fc kama Simba ingetumia vyema nafasi nyingi walizotengeneza

Mabao ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na Shomari Kapombe aliyefunga bao la mapema dakika ya 5 kabla ya Jean Charles Ahoua kuongeza la pili dakika ya 33 muda mfupi baada ya kuingia akichukua nafasi ya Awesu Awesu aliyeumia

Ahoua amefikisha mabao matatu akiwa ndiye kinara wa mabao kwa upande wa Simba akiwa pia na pasi nne za mabao

Msumari wa mwisho katika jeneza la Namungo Fc ulipigiliwa na kiungo Debora Mavambo na kuihakikishia Simba alama tatu muhimu zilizowasogeza hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi

Mambo bado ni magumu kwa Namungo Fc ambayo leo imepoteza mchezo wa tatu mfululizo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’