Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo kwa mechi tatu kupigwa katika viwanja mbalimbali
Baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo katika uwanja wa nyumbani, Tanzania Prisons leo wanashuka dimba la Sokoine kuikabili KMC
Pengine ni mechi ya kuamua hatma ya kocha Mbwana Makata kwani kama Prisons itakosa ushindi leo, kibarua chake kitakuwa mashakani
Mabingwa watetezi Yanga wako ugenini mkoani Arusha katika mchezo dhidi ya Coastal Union
Mechi nyingine inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini. Yanga ndio timu pekee ambayo imeshinda mechi zote bila ya kuruhusu bao msimu huu
Coastal Union wamejipata katika mechi za karibuni, leo watakuwa dimba la Sheikh Amri Abeid wakiongozwa na kocha Juma Mwambusi kusaka alama tatu mbele ya vijana wa kocha Miguel Gamondi
Dodoma Jiji na JKT Tanzania zitahitimisha ratiba ya leo kwa mechi itakayopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma saa 1 usiku



