Local,Normal News,Yanga, Coastal, Dodoma, Prisons, KMC, JKT

Yanga yaichapa Coastal Union, Prisons yapigwa nyumbani

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Oct 2024
Yanga yaichapa Coastal Union, Prisons yapigwa nyumbani

Bao la dakika ya 25 lililofungwa na Jean Beleke lililotosha kuihakikishia Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Maabad Maulid alikaribia kuifungia Coastal Union bao la mapema kama sio mpira wake wa kichwa kugonga mwamba kabla ya kuokolewa na walinzi wa Yanga

Mpira wa kona uliopigwa na Maxi Nzengeli ulipelekea piga nikupige langoni kwa Coastal Union kabla ya kumfikia Baleke aliyefunga

Yanga imeandikisha ushindi wa saba ikirejea nafas ya pili katika msimamo wa ligi. Aidha wananchi wameandikisha cleansheet ya saba pia

Katika mchezo uliopigwa mapema, Prisons ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa KMC nyumbani

Ni kipigo cha tatu mfululizo kwa Prisons, matokeo ambayo yanaweka mashakani kibarua cha kocha Mbwana Makata

Dodoma Jiji ikafanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
35m ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
19h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’