Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, Singida BS

Stars kamili kuikabili Sudan kusaka tiketi ya CHAN

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Oct 2024
Stars kamili kuikabili Sudan kusaka tiketi ya CHAN

Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, leo saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, kitajitupa kwenye Uwanja wa de la Capitale, jijini Nouakchott, nchini Mauritania kucheza mechi ya mtoano, kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za mataifa kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN). Kocha Mkuu wa timu hiyo Bakari Shime amesema wapo tayari kwa mapambano

Stars, inayoundwa na wachezaji wanaocheza hapa nchini, ipo chini ya kocha Shime, inacheza mechi hiyo nchini humo badala ya Sudan kutokana na nchi hiyo kuwa na machafuko ya vita kwa wenyewe kwa wenyewe

Kocha Shime amesema kila kitu ambacho kinahitajika kwa ajili ya mchezo huo, kimefanyika na kinachosubiriwa ni wachezaji wake kuingia uwanjani, ili wakalipambanie taifa

"Nawaamini vijana wangu, kuna watu wanasema wengi hawana uzoefu, ni kweli, lakini hawana uzoefu kwenye michezo ya kimataifa tu, lakini wana uzoefu wa kucheza kwenye klabu zao za Ligi Kuu, naamini wanaweza kwani hata wale ambao ni wazoefu walianza kama hawa," alisema Shime

Kati ya wachezaji 24 walioteuliwa kuunda kikosi hicho, 11 wanatoka timu ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes iliyotwaa Ubingwa wa CECAFA hivi majuzi nchini, kwa kuifunga Kenya mabao 2-1 katika mchezo wa fainali

Kuhusu kipa Aishi Manula, alisema yeye atakuwa kama kocha wa ndani na ndiyo maana amemchukua kwenye kikosi hicho

"Kwangu mimi kumchagua Manula nilichohitaji ni mdomo wake zaidi kuliko mikono yake. Hoja ni kwamba hajacheza muda mrefu, lakini Aishi yupo sawasawa, nafasi anayocheza ni ya golikipa na kama unavyoona wachezaji wote kwenye timu yetu wanaocheza nafasi ya ulinzi ni chipukizi, kwa hiyo wanamhitaji mtu nyuma yao ambaye anaweza kufanya kazi kama yangu mimi niliye kwenye benchi, namna gani anaweza kupeleka maelekezo sahihi na kuwafanya mabeki na wachezaji wote kucheza katika utaratibu unaotakiwa," alisema

Baada ya mechi hiyo, timu hizo zitacheza mchezo wa marudiano, Novemba 3, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Fainali za CHAN zinatarajiwa kufanyika hapa nchini, Uganda na Kenya, kuanzia Februari Mosi hadi 28 mwakani

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’