Transfer - International

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Oktoba 28 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Oct 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Oktoba 28 2024

Paris St-Germain wameungana na Real Madrid katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa kulia wa Liverpool Mwingereza Trent Alexander-Arnold, 26. (Fichajes – In Spanish)

Liverpool, wakati huo huo, wameulizia kuhusu beki wa kulia wa RB Salzburg Bosnia na Herzegovina Amar Dedic, ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Alexander-Arnold. (Caught Offside)

Wolves wamemfanya kiungo mkabaji wa Watford na Georgia Giorgi Chakvetadze, 25, kuwa mchezaji wanayemlenga mwezi Januari. (Sun)

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anaandaa misingi ya nani atakayechukua nafasi ya meneja Carlo Ancelotti msimu ujao huku akimpigia debe kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso. (Sport – in Spanish)

Mshambulizi wa zamani wa Italia Mario Balotelli, 34, amefanyiwa vipimo vya matibabu siku ya umatatu kabla ya kusajiliwa na klabu ya Serie A ya Genoa. (Fabrizio Romano)

West Ham wanavutiwa na mshambuliaji wa Atalanta na Nigeria Ademola Lookman, 27, huku meneja Julen Lopetegui akitumai kuimarisha safu yake ya mashambulizi mwezi Januari. (GiveMeSport)

Manchester City wanajiandaa kumpa mlinzi wa Croatia Josko Gvardiol, 22, mkataba ulioboreshwa wenye thamani ya £150,000 kwa wiki ili kuongeza muda wake wa kukaa Etihad Stadium kwa miaka miwili hadi 2030. (Star)

Kiungo mshambuliaji wa Uingereza na Chelsea Cole Palmer, 22, bado anajitolea kwa The Blues licha ya kuhusishwa na kutaka kuondoka, ikiwa ni pamoja na kurejea Manchester City. (Football Insider)

AC Milan wana nia ya kumpa winga wa Liverpool na Italia Federico Chiesa mwenye umri wa miaka 27 njia ya kurejea Serie A. (Caught Offside)

Beki wa zamani wa Ujerumani Mats Hummels, 35, anaweza kuondoka Roma mwezi Januari licha ya kujiunga na klabu hiyo ya Serie A kama mchezaji huru msimu wa joto. (Nicolo Schira)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’