Stars yaanza vibaya CHAN

Joel JJ By Joel JJ β€’ 28th October 2024


Stars yaanza vibaya CHAN

Timu ya Taifa ya Tanzania inayohusisha wachezaji wa ndani, imeanza vibaya kampeni ya kuwania kufuzu fainali za CHAN 2025 ikikubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Sudan katika mchezo uliopigwa huko Mauritania

Bao la dakika ya 23 lililofungwa na Mohammed Abdulrahman liliihakikishia Sudan ushindi huo wa nyumbani

Tanzania sasa itahitaji kushinda angalau mabao mawili ili kufuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda

Kama mwenyeji mwenza wa michuano hiyo, Tanzania inapaswa kupambana ili kuhakikisha inafuzu


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.