Local,Normal News,Yanga

Gamondi alalamikia viwanja ligi kuu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Oct 2024
Gamondi alalamikia viwanja ligi kuu

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, ameulalamikia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, akisema hauko kwenye ubora, huku akisema viwanja vitatu tu vinavyobeba taswira ya soka la Tanzania ni ule wa Benjamin Mkapa, Azam Complex, ambavyo vyote vipo, Dar es Salaam na New Amaan Complex, Zanzibar

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya timu yake na Coastal Union, akiibuka na ushindi wa bao 1-0 lililowekwa wavuni na Jean Baleke, Gamondi amesema, baadhi ya viwanja ni vibovu kiasi kwamba vinasababisha timu zicheze mpira wa kubutuabutua kitu ambacho si picha nzuri kwa Ligi ya Tanzania

"Pointi hizi tatu ni muhimu sana kwetu katika mwendelezo wa kupigania nafasi ya kutwaa ubingwa, lakini sijafurahishwa na hali ya uwanja, pamoja na baadhi ya maamuzi ya mwamuzi"

"Kwa wachezaji wakubwa na ligi bora huwezi kucheza mpira kwenye uwanja kama huu, haikuwa mbaya kwa upande wetu, hata Coastal Union walikuwa wakipiga mipira mirefu, walijaribu kama mara mbili tatu kuanzia mpira nyuma wakashindwa na kuanza kubutua na hii si picha nzuri kwa Ligi ya Tanzania"

"kwangu mimi, Uwanja wa Azam Copmlex, New Amaan Zanzibar na Benjamin Mkapa, ndivyo vinavyobeba taswira njema ya ligi ya hapa nchini," alisema kocha huyo

Baada ya ushindi huo, Yanga inaelekea Zanzibar kwa ajili ya mchezo mwingine dhidi ya Singida Black Stars utakaopigwa Jumatano Oktoba 30 katika uwanja wa New Amaan Complex

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’