Kocha wa zamani wa Manchester City, Muitaliano Roberto Mancini amefutwa kazi kwenye kibarua chake cha timu ya taifa ya Saudi Arabia
Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 59 aliteuliwa kwenye kiti hicho Agosti 2023 na kusaini mkataba wa miaka minne uliokuwa na thamani ya Pauni 77 milioni. (Sh 272bilioni)
Mkataba huo ulimfanya Mancini kuwa kocha ghali zaidi duniani. Lakini, maisha yake huko Mashariki ya Kati yalikuwa kwenye wakati mgumu
Mancini alipata ushindi mara saba tu katika mechi 18 alizoiongoza timu hiyo katika kipindi cha miezi 14 aliyokuwa kazini