Bodi ya Ligi imeahirisha mechi mbili za ligi kuu zinazoihusisha klabu ya JKT Tanzania ambayo jana ilipata ajali wakati ikitokea mkoani Dodoma
Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Karim Boimanda amesema mchezo kati ya Simba dhidi ya JKT Tanzania uliokuwa upigwe kesho Jumanne katika uwanja wa KMC Complex umeahirisha pamoja na mchezo uliokuwa ukifuata kati ya JKT Tanzania dhidi ya Namungo Fc
JKT Tanzania walipata ajali jana Mbweni jijini Dar es salaam wakitokea Dodoma ambako walicheza mechi dhidi ya Dodoma Jiji na timu kuondoka usiku baada ya mchezo ili kuwahi mchezo uliokuwa ukifuata dhidi ya Simba
Wachezaji 11 waliumia katika ajali hiyo na wako chini ya uangalizi wa madaktari