Fountain Gate imeanza vyema msimu huu ligi kuu ya NBC ikishika nafasi ya tano baada kwenye msimamo wa ligi baada ya kukusanya alama 17
Kama utazungumzia mafanikio ya Fountain Gate msimu huu basi hutakosa kutaja jina la kiungo mshambuliaji Salum Kihimbwa
Kihimbwa amehusika katika mabao saba yaliyofungwa naa timu hiyo akifunga mabao matatu na kutoa assist nne
Jana alibeba tuzo ya nyota wa mchezo dhidi ya Mashujaa Fc akifunga bao la pili la Fountain Gate katika mchezo ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
Kihimbwa, Selemani Mwalimu, William Edgar na Dickson Ambundo wamekuwa chachu ya mafanikio ya kikosi cha Fountain Gate msimu huu



