Timu ya Serie A ya Italia iliyokumbwa na majeraha Genoa ilitangaza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Italia Mario Balotelli siku ya Jumatatu
Genoa ina wachezaji saba ambao ni majeruhi akiwemo fowadi Junior Messias, Vitinha na Caleb Ekuban na wameamua kucheza kamari kwa mchezaji huru Balotelli, ambaye alicheza mara ya mwisho Serie A akiwa na Brescia miaka minne iliyopita na msimu uliopita alikuwa Adana Demirspor nchini Uturuki
"Balotelli ni mchezaji mpya wa Genoa, karibu Super Mario" ilithibitisha klabu hiyo inayoshika nafasi ya 18 baada ya Jumapili kufungwa 3-0 na Lazio
Balotelli amesaini hadi mwisho wa msimu huu, vyombo vya habari vya Italia viliripoti
Mzaliwa wa Palermo kwa wazazi wa Ghana, alikuwa mmoja wa nyota wachanga wa soka ya Italia na kuchukuliwa kuwa mshambuliaji wa kiwango cha dunia, akichezea Inter Milan, Manchester City, AC Milan na Liverpool
Lakini msururu wa vilabu vidogo ulifuata na, akiwa na umri wa miaka 34, kuhamia Genoa kunawakilisha nafasi ya mwisho kwa Balotelli kwenye hatua kubwa baada ya kazi ngumu ambapo vichwa vya habari vya nje ya uwanja vimekuwa jambo la kawaida kwake



