Local,Normal News,Yanga, Singida

Yanga yaifuata Singida BS Zanzibar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Oct 2024
Yanga yaifuata Singida BS Zanzibar

Msafara wa kikosi cha Yanga umeondoka jijini Dar es salaam mapema leo kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars ambao utapigwa kesho Jumatano, Oktoba 30 katika uwanja wa New Amaan Complex

Wakati Yanga wakielekea Zanzibar leo, wapinzani wao Singida BS wako Zanzibar tangu juzi wakiendelea na maandalizi ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa wanakwenda Zanzibar kuchukua alama tatu kwani wapinzani wao wamefanya makosa kupeleka mchezo huo Zanzibar ambako ni ngome yao

Kumekuwa na vita ya maneno baina ya wasemaji wa timu hizo Kamwe na Hassan Massanza ambaye jana alitoa tahadhari kuwa hawapaswi kwenda na matokeo yao mfukoni

Mchezo huo unazikutanisha timu mbili zenye rekodi bora katika ligi kuu msimu huu

Singida Black Stars wako kileleni mwa msimamo wa ligi wakikusanya alama 22 baada ya kushinda mechi saba na kutoka sare mchezo mmoja

Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 21 baada ya kucheza mechi saba na kushinda zote pasipo kuruhusu bao

Dakika 90 za mchezo wa kesho zitaamua kama ni Yanga inayokwenda kukaa kileleni kama itaibuka na ushindi au ni Singida BS watakaobaki hapo kama watashinda au hata kutoka sare

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’