Ligi Kuu ya NBC iliendelea leo kwa mechi mbili kupigwa mikoa ya Mbeya na Arusha
Wakitumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid kama uwanja wao wa nyumbani, Coastal Union wameichapa Kagera Sugar bao 1-0
Wagosi hao wa Kaya walilazimika kuzubiri mwishoni mwa kipindi cha pili kujihakikishia alama tatu kwa bao la dakika ya 86 lililofungwa na Semfukwe Charles

Ni ushindi ulioisogeza Coastal Union hadi nafasi ya nane katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 11
Mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya kati ya KenGold dhidi ya Dodoma Jiji ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
KenGold walinusurika na kpigo katika mchezo huo wakisawazisha bao la pili dakika ya 90 kupitia kwa Mishamo Daudi aliyefunga mabao yote mawili
Mabao ya Dodoma Jiji yalifungwa na Dissan Galiwango na Zidane Sereli
Dodoma Jiji wamesalia nafasi ya 7 katika msimamo wakiwa na alama 13 huku KenGold wakiendelea kubaki mkiani wakiwa na alama 5



