Juzi Pamba Jiji ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Namungo Fc, katika mchezo wa raundi ya 10 ligi kuu ya NBC
Kipigo hicho kimeendeleza mlolongo wa matokeo mabovu ya timu hiyo tangu ilipopanda daraja msimu huu
Ikiwa imeshacheza michezo 10, Pamba Jiji haijashinda hata mchezo mmoja ikiwa ni timu pekee ambayo haijaonja utamu wa ushindi kwenye Ligi Kuu
Wamepoteza michezo mitano na sare tano wakishika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu wenye timu 16, ikiwa ina pointi tano tu mpaka sasa, ikiizidi KenGold kwa tofauti ya mabao tu
Pamba Jiji kwa sasa inanolewa na kocha Freddy Felix Minziro ambaye ameiongoza timu hiyo katika mechi mbili na kuambulia alama moja tu