Nyota wa Hispania Alvaro Morata amesisitiza kuwa AC Milan inaweza kujivunia kiwango chao licha ya kupoteza mchezo wa Serie A dhidi ya Napoli Jumanne usiku
Romelu Lukaku na Khvicha Kvaratskhelia walifunga mabao ya Napoli ikishinda 2-0 kwenye Uwanja wa San Siro
Mshambuliaji huyo wa Milan Morata alizungumza baada ya mchezo huo uliorushwa mbashara na Azam TV
"Kandanda ni kama hii, tunapaswa kuwa chanya. Tulikuwa na wakati mzuri dhidi ya timu ya juu kwenye ligi. Lakini lazima tukubali"
"Tulicheza mchezo mzuri tukiwapa wakati mgumu wapinzani wetu. Wamezoea kupata nafasi nyingi zaidi, lakini leo wamepiga mashuti mawili na kufunga mabao mawili"
"Tutarudi tukiwa imara zaidi ili tuweze kushinda mechi zinazofuata. Ninajivunia sana uchezaji wa kila mtu, tulionyesha nguvu na hamu ya kushinda. Tuliruhusu mabao mawili kwa makosa madogo," alisema