Klabu ya Yanga imeanza mazungumzo ya kuhuisha mikataba ya nyota wake wa kikosi cha kwanza raia wa Ivory Coast Pacome Zouzoua na Yao Kouassi, imefahamika
Yao na Pacome ni miongoni mwa wachezaji katika kikosi cha Yanga ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu kama ilivyo kwa kiungo Mganda Khalid Aucho
Mapema wiki hii zilivuna tetesi kuwa klabu ya Simba inafuatilia kwa ukaribu upatikanaji wa wachezaji hao ambao ifikapo Disemba wataruhusiwa kuzungumza na timu yoyote kwa kuwa mikataba yao itakuwa chini ya miezi sita
Hata hivyo habari ya uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga ni kuwa Wananchi wamepiga hatua kubwa katika majadiliano ya kuwaongeza mikataba
Wakala wa wachezaji hao Zambro Traore tayari yuko nchini kukamilisha mazungumzo na Yanga kwa niaba ya wateja wake
Zambro anatarajiwa kushuhudia mchezo wa ligi kuu leo kati ya Singida Black Stars dhidi ya Yanga utakaopigwa uwanja wa New Amaan Stadium baadae leo
Zambro anawasimamia wachezaji wengine kama Stephane Aziz Ki na Joseph Guede ambaye kwa sasa anaitumikia Singida BS




