Bao la dakika ya 67 lililofungwa na Pacome Zouzoua limeipeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars
Ilikuwa mechi kali iliyojaa ufundi pamoja na ubabe kutoka kwa kila timu, vita halisi ya juu ya msimamo wa ligi
Yanga walionekana kutawala mchezo katika kipindi cha kwanza huku Singida BS wakifanya mashambulizi yao kwa kushitukiza zaidi
Mashambulizi makali yalitengenezwa na kila timu katika kipindi cha pili lakini walikuwa ni Yanga walionufaika na shuti la nje ya 18 kutoka kwa Pacome
Yanga imefikisha alama 24 ikiishusha Singida BS nafasi ya pili katika msimamo wa ligi