KMC mikononi mwa Namungo NBC PL

Joel JJ By Joel JJ β€’ 31st October 2024


KMC mikononi mwa Namungo NBC PL

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mchezo mmoja kati ya KMC dhidi ya Namungo Fc utapigwa uwanja wa KMC Comlex, Kinondoni jijini Dar es salaam

Ni mechi itakayozikutanisha timu mbili ambazo zimezinduka zikitoka kushinda mechi zao zilizopita

KMC waliichapa Prisons mabao 2-1 katika mchezo uliopita wakati Namungo Fc ambayo inanolewa na kocha Juma Mgunda, iliichapa Pamba Jiji bao 1-0

Kama KMC itaibuka na ushindi katika mchezo huo unaweza kusogea hadi nafasi ya sita katika msimamo sasa ikiwa ya 9 ikikusanya alama 11

Namungo wameshinda mechi tatu tu msimu huu, wakishika nafasi ya 12 na alama zao 9


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.