Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Novemba 1 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Nov 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Novemba 1 2024

Sporting wamefikia makubaliano ya kumruhusu meneja Ruben Amorim kuondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Manchester United wakati wa mapumziko ya kimataifa ya Novemba. (Telegraph - Subscription Required)

United italipa fidia kuwezesha idadi ya wafanyikazi wa Amorim kuungana naye Old Trafford. (ESPN)

Mshambulizi wa Uswidi Viktor Gyokeres, 26, na kiungo wa kati wa Denmark Morten Hjulmand, 25, hawajafurahishwa na uamuzi wa Amorim kuondoka Sporting baada ya kukataa ofa ya kuondoka klabuni hapo msimu uliopita. (Ojogo - In Portugal )

Lakini Gyokeres huenda akajiunga na Amorim katika klabu ya Manchester United iwapo makubaliano yatakubaliwa. (Soka365)

Mshambulizi wa Bayern Munich na Ujerumani Jamal Musiala, 21, anasema ana furaha katika klabu hiyo ya Bundesliga huku akihusishwa na uhamisho wa kujiunga na Manchester City. (Goal)

Manchester United wanaweza kushindana na Liverpool kwa ajili ya kumnunua beki wa pembeni wa Wolves wa Algeria Rayan Ait-Nouri. (GiveMeSport)

Brentford itadai pauni milioni 60 kumnunua mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25, katika dirisha la uhamisho la Januari huku Arsenal ikiwa na nia ya kutaka kumnunua. (Football Insider)

Steven Gerrard anakabiliwa na shinikizo la kufutwa kazi kama meneja wa Al-Ettifaq baada ya kiwango duni cha klabu hiyo ya Saudia kusababishwa na kutolewa kwao katika kikombe wiki hii. (Sun)

Kikundi cha uwekezaji wa michezo duniani kinafahamika kuwa kilitoa ofa ya 45% ya hisa katika Crystal Palace. (Mail)

Aston Villa wako kwenye mazungumzo na fowadi wa Uingereza Morgan Rogers, 22, kuhusu mkataba mpya. (Athletic - Subscription Required)

Real Madrid wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa Aurelien Tchouameni, 24. (Relevo - In Spanish)

Real Madrid wako tayari kulipa £84m kwa Enzo Fernandez au wamtoe Tchouameni kwa Chelsea kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 23. (Fichajes, kupitia TeamTalk)

Barcelona wanafuatilia hali ya Rafael Leao huko AC Milan kwa nia ya kumnunua winga huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 25 msimu wa joto. (Sport - In Spanish)

Liverpool wamemtambua mlinzi wa Bournemouth na Hungary Milos Kerkez, 20, kama mgombea katika kutafuta beki mpya wa kushoto. (TeamTalk)

Athletic Bilbao wanatumai kukubaliana mkataba mpya na winga wa Uhispania Nico Williams, 22, huku kukiwa na hamu kutoka kwa Barcelona. (Sport - in Spanish)

Getafe wanatazamia kutaka kumnunua beki wa Tottenham Mhispania Sergio Reguilon, 27, ambaye mkataba wake unamalizika Juni 2025. (Fichajes - In Spanish )

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
1h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
1h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
2h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
3h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
4h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
6h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
8h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
9h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
10h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
11h ago
READ MORE β†’