Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc wametakata uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Pengine ni matokeo ya kikatili kwa Mashujaa Fc ambao jitihaza zao za angalau kupata alama moja katika mchezo huo zilipotea kwenye dakika ya 96 kwa bao la Steven Mukwala
Mpira wa kona uliochongwa na Awesu Awesu ulimkuta Mukwala akiwa hajakabwa baada ya walinzi wa Mashujaa kuzubaa na Mganda huyo kuujaza mpira kimiani
Simba ilitengeneza nafasi nyingi zaidi lakini kukosa umakini na uimara wa mlinda lango Erick Johora uliiweka Mashujaa mchezoni kwa muda mrefu
Ni ushindi ambao umeisogeza Simba katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 22 sawa na Singiida Black Stars ambao wamezidiwa mabao
