Yanga yakumbana na rungu la Bodi ya Ligi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Nov 2024
Yanga yakumbana na rungu la Bodi ya Ligi

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imeitoza klabu ya Yanga fainai ya jumla ya Tsh Milioni 12 kutokana na makosa yaliyojitokeza katika mechi zilizopita

Yanga imetozwa faini ya Sh 10 Milioni kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi kuingia Uwanjani siku ya mchezo dhidi ya Simba kinyime na kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo

Yanga pia imetozwa faini ya Sh1 Milioni kwa kosa la kukataa kutumia chumba maalumu cha kubadilishia Nguo kwenye Uwan-ja wa Mkapa kinyume na kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo

Yanga imetozwa faini ya Sh 1Milioni kwa kosa la kuwakiliswa na kocha Mkuu pekee kwenye mkutano wa Wanahabari kueleke mchezo huo kinyume na natakwa ya kanuni ya 17:58 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo inayotaka aambatane na nahodha ama mchezaji mwenye ushawishi Kikosini

Aidha vinara hao wa ligi pia wamepewa onyo kwa kuchelewa kuingia uwanja kwa dakika 15 kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba

Katika hatua nyingine, Meneja wa Yanga, Walter Harrison amefungiwa michezo mitatu na faini ya Sh 1 milioni kwa kosa la kuwashurutisha waamuzi waliochezesha mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union kufanya maamuzi kwa mujibu wa wa maoni yake

Katika mchezo huo Walter alitumia kopyuta ndogo kuwaonesha marudio ya picha mjongeo (video) ya matukio mbalimbali ya mchezo huo kama ushahidi wa yale aliyokuwa akiyalalamikia

Kitendo hicho kimetafsiriwa na kamati kama kinachoweza kushawisi shari au vurugu uwanjani

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
40m ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
2h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
3h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
3h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
5h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
6h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
6h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
18h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’