Meneja wa Manchester United Ruben Amorim anataka kumchukua beki wa kati wa Sporting mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ivory Coast Ousmane Diomande, ambaye anakadiriwa na kiwango cha thamani ya pauni milioni 70, kwenda naye Manchester United. (Sun)
Mshambulizi wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres anaendelea kulengwa na Arsenal na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 sasa anafikiria chaguo lake baada ya kuondoka kwa Amorim - huku kukiwa na uwezekano wa kuhamia London. (TeamTalk)
Manchester United wanaweza kuungana na mahasimu wao wa Primia Ligi Arsenal , Chelsea , Liverpool na Manchester City katika mbio za kumsajili Gyokeres. (Florian Plettenberg, Sky Sports Germany)
Manchester United ni miongoni mwa vilabu vitatu vikubwa barani Ulaya vinavyomfuatilia mshambuliaji wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 24 Vinicius Jr, huku ofa ya kandarasi ya euro bilioni moja ikiwa ikijadiliwa. (Relevo, kupitia TeamTalk)
Kiungo wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza Steven Gerrard ameapa kupambana kuendelea kuwa meneja wa Al-Ettifaq baada ya wito wa kumtaka ajiuzulu nafasi hiyo. (Mail)
Kikosi cha kwanza cha Manchester United kinatamani sana meneja wa muda wa Uholanzi Ruud van Nistelrooy aendelee kubakia katika klabu hiyo baada ya Amorim kuchukua mikoba ya Old Trafford. (Sun)
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumsajili winga wa Bayern Munich wa Ujerumani, Leroy Sane, 28. (Christian Falk, Bild)
The Gunners na klabu nyingine ya Primia Ligi Southampton wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Palmeiras mwenye umri wa miaka 18 Luighi. (Nosso Palmeiras - in Portuguese)
Kocha mkuu wa Chelsea Enzo Maresca anakabiliwa na kizingiti kikubwa iwapo anataka kumchukua beki wa Denmark Patrick Dorgu mwenye umri wa miaka 20 kwenda Stamford Bridge, kwani nyota huyo wa Lecce yuko mbioni kusalia Serie A. (GiveMeSport)
Mkufunzi wa Wolves Gary O'Neil ana michezo miwili pekee kuokoa kibarua chake baada ya kuanza vibaya msimu huu. (Football Insider)
BBC



