Local,Normal News,Yanga, Azam, Singida, Coastal

Ni Yanga vs Azam Fc, Dar Derby

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Nov 2024
Ni Yanga vs Azam Fc, Dar Derby

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi mbili zinatarajiwa kupigwa jijini Dar es salaam na kule visiwani Zanzibar

Yanga itakuwa mwenyeji wa Azam Fc katika Derby ya Dar es salaam, mchezo ukitarajiwa kupigwa uwanja wa Azam Complex saa 12 jioni na kufuatiwa na mchezo kati ya Singida Black Stars dhidi ya Coastal Union utakaopigwa uwanja wa New Amaan Complex, saa 2:30 usiku

Macho na masikio ya mashabiki wengi wa soka yameelekezwa kule Azam Complex ambao mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc utapigwa

Yanga na Azam Fc zimetoa mechi bora yenye ushindani katika misimu ya karibuni. Wengi wanaamini ukitoa derby ya watani wa jadi, Derby ya Dar kati ya Yanga na Azam Fc ni mchezo wa pili wenye mvuto zaidi

Wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, Yanga wataingia katika mchezo huo wakizisaka alama tatu ili waendelee kutimua vumbi pale juu

Hata hivyo haitakuwa kazi rahisi mbele ya Azam Fc, timu pekee iliyoifunga Yanga kwenye ligi mwaka 2023

Ndio! March 17 2023 Azam Fc iliichapa Yanga mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Tangu wakati huo, Yanga haijapoteza mchezo wowote ndani ya ligi kuu wakicheza mechi 17, kushinda mechi 16 na kutoka droo mechi moja

Ushindi au hata sare kwa Azam Fc mbele ya Yanga leo utaweka rekodi nyingine kwa matajiri hao wa Chamazi pengine kuwa timu ya kwanza kuizuia Yanga msimu huu

Ikumbukwe msimu huu Yanga imeshinda mechi zote nane, ikifunga mabao 13 pasipo kuruhusu bao upande wao

Ni wazi Azam Fc watahitaji kuwa kwenye ubora wao, kuizuia Yanga ambayo mapema msimu huu ilibeba Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam Fc

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
29m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’