Azam Fc yamaliza ubabe wa Yanga NBC PL

Joel JJ By Joel JJ β€’ 2nd November 2024


Azam Fc yamaliza ubabe wa Yanga NBC PL

Azam Fc imetakata uwanja wa Azam Complex ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo mkali wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Azam Complex

Azam Fc ilionekana kusaka ushindi mapema kwa kufanya mashambulizi mfululizo katika lango la Yanga

Makosa ya Ibrahim Bacca kumvuta Saadun aliyekuwa anaelekea langoni kuonana na Djigui Diarra yaliigharim Yanga baada ya beki huyo kuonyeshwa kadi nyekundu

Kutolewa kwa Bacca kuliifanya Azam Fc itawale mchezo huo na hatimaye Gibril Sillah akafunga bao dakika chache baadae baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Mtasingwa

Baada ya kufanga bao hilo Wananchi wakazinduka kusaka bao la kusawazisha hata hivyo walishindwa kuipenye ngome ya Azam Fc iliyokuwa ikilindwa na wachezaji 10 nyuma ya mpira

Ni ushindi uliomaliza rekodi ya Yanga kutopoteza mchezo au kuruhusu bao msimu huu

Upande wa Azam Fc ni furaha kwao kwani wameifunga Yanga kwnye ligi 'back 2 back'


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.