Real Madrid wanavutiwa sana na beki wa Liverpool na Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, wanapojiandaa kuimarisha safu yao ya ulinzi. (AS - kwa Kihispania)
Newcastle United wamemjumuisha winga wa Cameroon Bryan Mbeumo kwenye orodha ya wachezaji wanaowataka, huku Brentford ikiweka bei ya pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)





