Local,Normal News,Simba

Manula haumii kutocheza Simba?

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Nov 2024
Manula haumii kutocheza Simba?

Mlinda lango wa Simba Aishi Manula amesema licha ya kutopata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, anashirikiana vyema na wenzake katika kuhakikisha timu inafikia malengo ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Jana Manula aliiongoza timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kwa wachezaji wa ndani katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za CHAN 2025 Tanzania ikipoteza kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya sare ya bao 1-1 (aggregate)

Manula amesema anafuraha kuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu huu licha ya kutoonekana mara kwa mara uwanjani

"Nimekuwa nikifanya mazoezi ndani ya Simba chini ya makocha bora, hivyo hata kama sichezi nimekuwa katika ubora na utimamu mzuri ndio maana nimepata nafasi kuitumikia timu ya Taifa"

"Ninashirikiana vyema na wenzangu hata kama sionekani uwanjani nikicheza, kama timu tuna lengo moja, haijalishi nani anaanza lakini dhamira yetu ni kuona tunatimiza lengo la kutwaa ubingwa"

"Nafurahi nimepata nafasi ya kuonyesha nilichonacho timu ya Taifa, nitaendelea kupambana kwani naamini wakati utafika nitacheza," alisema Manula

Msimu huu Manula alipata nafasi ya kuichezea Simba katika mechi moja ya kirafiki dhidi ya Al Hilal iliyomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Imekuwa si rahisi kwake kupenya katika kikosi cha kwanza mbele ya Moussa Camara, Ali Salim na hata Ayoub Lakred ambaye amerejea hivi karibuni baada ya kuwa nje kwa miezi kadhaa akiuguza majeraha

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’