Local,Normal News,Pamba

Mpole ana matumaini mapya Pamba Jiji

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Nov 2024
Mpole ana matumaini mapya Pamba Jiji

Mshambuliaji wa Pamba Jiji George Mpole amesema licha ya kipindi kigumu ambacho timu hiyo inapitia, watarejea katika ubora na kufanya vizuri katika mechi zilizosalia ligi kuu ya NBC msimu huu

Pamba Jiji inashika nafasi ya 15 katika ligi kuu ya NBC ikikusanya alama 5 kutoka mechi 10

Pamba Jiji ambayo sasa inanolewa na Kocha Freddy Felix Minziro haijashinda mchezo wowote msimu huu

Mpole amesema kama mchezaji anatamani kuona timu hiyo inafanya vizuri, lakini halitawezekana kama hawatapambana katika mechi zilizosalia ili kuhakikisha wanajinusuru kurudi Ligi ya Championship

Mpole amesema jambo muhimu kwao ni kuona wanaanza kushinda mechi na kuongeza morali ya timu

"Tukianza kushinda mechi kujiamini kutaongezeka, morali itakuwa juu, ndio maana tunaendelea kupambana na kuhamasishana hadi tutakapoanza kukaa katika mstari"

"Kwa upande wangu kama mshambuliaji napambana naona ni suala la muda kuanza kuhesabu mabao yangu. Sijawahi kukata tamaa na siyo mtu wa kukata tamaa ninapofanya jambo lolote," alisema Mpole

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’