Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo Novemba 05 ambapo mchezo mmoja utapigwa kule Manyara
Fountain Gate watakuwa wenyeji wa Pamba Jiji katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Kwaraa, Babati
Wenyeji Fountain Gate wamekuwa na mwanzo mzuri katika ligi msimu huu wakishika nafasi ya 5 baada ya kucheza mechi 10 na kukusanya alama 17
Wanakutana na Pamba Jiji ambao hawajui radha ya ushindi katika ligi msimu huu. Pamba wanashika nafasi ya 15 wakiwa na alama tano tu
Vijana hao kocha Fleddy Felix Minziro wanapaswa kuanza kukusanya alama zaidi sasa kama hawataki kurejea katika ligi ya Championship msimu ujao