International,Normal News,Real Madrid, PSG, France

Mbappe, Rais PSG bado hakieleweki

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Nov 2024
Mbappe, Rais PSG bado hakieleweki

Ugomvi baina ya staa wa Real Madrid, Kylian Mbappe na rais wa Paris Saint-Germain, Nasser Al-Khelaifi unadaiwa kuwa bado unaendelea huku moja ya sababu ni kile ambacho rais huyo alifanya kwa mdogo wake Mbappe

Al-Khelaifi na Mbappe walikuwa na panda shuka nyingi kwa msimu uliopita baada ya staa huyo kugoma kusaini mkataba mpya na kuwaambia kuwa ataondoka, jambo ambalo lilimkera tajiri huyo aliyekuwa akihitaji kuendelea kuwa naye

Mara kadhaa Mbappe aliondoshwa katika kikosi cha kwanza huku ripoti zikifichua Nasser alishajua kwamba Mbappe ameshafikia makubaliano na Madrid

Inaelezwa ugomvi baina ya wawili hawa ulienda mbali ukahusisha hadi familia na wakati fulani Nasser Al-Khelaifi alitoa amri kwa kocha Luis Enrique kuwa asimjumuishe mdogo wake Mbappe aitwaye Nathan katika kikosi cha wakubwa, tukio lililotokea wakati msimu uliopita unaelekea mwishoni

Kwa mujibu wa tovuti ya L'Equipe, Mbappe alimkuta Ethan akilia ndani ya chumba cha kubadilishia nguo baada ya kutemwa katika timu hali iliyozidisha hasira kwa Mbappe ambaye alienda kujibizana na Al-Khelaifi juu ya suala hilo

Mbappe hakupendezwa na tabia za rais huyo na akamwambia kwamba hatokaa asamehe Euro 55 milioni ambazo zimetokana na mshahara anaoidai timu hiyo ambazo hakuwa analipwa baada ya kuondolewa kwenye timu kutokana na barua yake ya kuwataarifu kuwa hataongeza mkataba

Wakati Mbappe anaelekea Madrid, mdogo wake alijiunga na Lille ambako tangu kuanza kwa msimu huu hajafanya vizuri akicheza mechi nne tu na sababu kubwa ikieleza kuwa ni majeraha

Mbappe aliishtaki PSG kuhusu mshahara wake, kesi ambayo alishinda lakini PSG ikagoma kulipa na inataka kupelekea kesi mahakama ya juu zaidi

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’